Orodha ya Masomo
-
Somo la 1: Mimi ni Anna.
Anna ni mwanafunzi kutoka Thailand. Leo anakutana na mwelekezi wake Sakura kwa mara ya kwanza katika chuo kikuu.
-
Somo la 2: Hii ni nini?
Anna, mwanafunzi kutoka Thailand, alijitambulisha kwa Sakura, mwelekezi wake. Anna anampa Sakura kitu.
-
Somo la 3: Msalani ni wapi?
Leo, Sakura anamtembeza Anna Chuoni.
-
Somo la 4: Nimerudi hivi sasa.
Anna amerudi bwenini na Sakura. Msimamizi wa bweni amekuja mlangoni kuwasalimia.
-
Somo la 5: Hizo ni hazina zangu.
Anna amemwalika Sakura kwenye chumba chake bwenini. Sakura aliona kitu.
-
Somo la 6: Namba yako ya simu ni ipi?
Anna na Sakura wanaendelea na mazungumzo yao chumbani mwa Anna. Sakura anamwuliza Anna namba yake ya simu.
-
Somo la 7: Kuna skonzi za krimu?
Anna na Sakura wamefika kwenye duka la kuuza keki.
-
Somo la 8: Rudia tafadhali.
Anna anahudhuria somo la Kijapani linaloongozwa na Profesa Suzuki katika chuo kikuu.
-
Somo la 9: Kuanzia saa ngapi?
Leo, Profesa Suzuki atatoa tangazo darasani.
-
Somo la 10: Je, wote wapo?
Leo, Anna atafanyiwa uchunguzi wa afya katika chuo chake. Wanafunzi wamekusanyika katika eneo la kufanyiwa uchunguzi.
-
Somo la 11: Tafadhali fanya kila namna ufike.
Karamu itafanyika katika bweni ambalo wanafunzi wa kigeni wanaishi akiwemo Anna. Anna anamkaribisha Sakura kwenye karamu.
-
Somo la 12: Ulikuja lini nchini Japani?
kuna karamu inayofanyika katika bweni la wanafunzi wa kigeni ambako Anna anaishi. Anamtambulisha Rodrigo, mwanafunzi mwenzake kutoka Mexico, kwa SAKURA.
-
Somo la 13: Ninapenda riwaya.
Anna, Sakura na Rodrigo wanaendelea na mazungumzo kwenye karamu, inayofanyika kwenye bweni la wanafunzi wa kigeni.
-
Somo la 14: Naweza kutupa taka hapa?
Anna anafanya usafi baada ya karamu iliyofanyika katika bweni lao.
-
Somo la 15: Wamelala.
Anna anaelekea katika duka la kuuza vitabu pamoja na Sakura na Rodrigo. Treni inayowabeba itawasili katika kituo cha Shinjuku muda mfupi kutokea sasa.
-
Somo la 16: Tafadhali panda ngazi, na uelekee upande wa kulia.
Anna amefika kwenye duka la kuuza vitabu ambalo liko Shinjuku pamoja na rafiki zake. Anna anamwuliza muuzaji upande ulio na katuni za manga.
-
Somo la 17: Pendekezo lako ni lipi?
Kwenye duka la vitabu, Anna ameona vitabu vingi vya manga ambavyo vinaonekana kumvutia. Hawezi kuamua ni kipi atakachokinunua.
-
Somo la 18: Nimepotea njia.
Anna alitembelea duka la kuuza vitabu pamoja na rafiki zake, Sakura na Rodrigo. Baada ya kuondoka kwenye duka hilo, Anna alipoteleana na wenzake.
-
Somo la 19: Ilikuwa vizuri.
Anna alipoteana na rafiki zake na kumpigia simu Sakura ili amusaidie. Je Anna atajumuika tena na Sakura na Rodrigo?
-
Somo la 20: Umewahi kuimba nyimbo za Kijapani?
Anna na wenzake, Sakura na Rodrigo wamefika kwenye kibanda cha Karaoke.
-
Somo la 21: Hapana, siyo sana.
Katika kibanda cha Karaoke, Anna ameimba wimbo wa Kijapani. Sakura anamsifu Anna kwa uimbaji wake mzuri.
-
Somo la 22: Nimechelewa.
Anna alifurahia katika kibanda cha Karaoke na rafiki zake kiasi kwamba alirejea bwenini akiwa amechelewa.
-
Somo la 23: Nilikaripiwa na mama msimamizi wa bweni.
Anna alipokuwa akiongea na Sakura chuoni, aliulizwa kuhusiana na siku aliporudi bwenini kwa kuchelewa.
-
Somo la 24: Tafadhali msitumie.
Anna anahudhuria darasa la somo la Kijapani ambalo Profesa Suzuki anafundisha. Prof. Suzuki anaelezea juu ya jaribio la wiki ijayo.
-
Somo la 25: Ingia chini ya dawati.
Anna amehudhuria darasa la somo la Kijapani na jengo la shule likaanza kutikisika.
-
Somo la 26: Tujitahidi wakati mwingine.
Leo, Anna amepata matokeo ya mtihani wa Kijapani. Alimuona mwanafunzi mwenzake Rodrigo akiwa ameinamisha kichwa chake.
-
Somo la 27: Nani anayeolewa?
Anna amemtembelea rafiki yake Sakura nyumbani mwake. Sakura alimuonyesha Anna kadi ya mwaliko wa harusi.
-
Somo la 28: Karibu Shizuoka.
Anna amefika mji wa Shizuoka na Sakura. Kenta ambaye ni binamu wa Sakura, yuko katika kituo cha treni ili akutane nao.
-
Somo la 29: Tukiangalia kwa karibu, unaonekana mkubwa, au siyo?
Anna ametembelea mji wa Shizuoka. Leo amepelekwa katika eneo mwafaka la kuutazama mlima Fuji pamoja na Kenta.
-
Somo la 30: Ningependa kupiga picha zaidi kidogo.
Anna alipokuwa akipiga picha za Mlima Fuji akiwa na Sakura na Kenta kukaanza kunyesha.
-
Somo la 31: Tayari nina umri wa miaka 82.
Anna ametembelea nyumbani kwa bibi yake Sakura, jijini Shizuoka. Bibi anaishi peke yake, na anatunza shamba dogo.
-
Somo la 32: Napenda zaidi futoni.
Anna atalala katika nyumba ya bibi yake Sakura. Hii ni mara yake ya kwanza kulala kwenye futoni, ambalo ni godoro la kijapani na matandiko yake.
-
Somo la 33: Anna, nitakupatia.
Anna amekwenda kwenye tamasha la chuo kikuu pamoja na Kenta ambaye ni binamu yake Sakura. Wanaangalia maonyesho ya picha yaliyoandaliwa na klabu ya upigaji picha.
-
Somo la 34: Ni laini na mtamu.
Baada ya Anna kuhudhuria tamasha la chuoni na Kenta, wawili hao wamekwenda kwenye mgahawa wa sushi ulio na mkanda wa kubebea chakula.
-
Somo la 35: Naweza kutumia kadi ya kufanyia manunuzi?
Anna pamoja na Kenta, walifurahia mlo wa sushi katika mgahawa wenye mikanda ya kubebea chakula.
-
Somo la 36: Napaswa kusoma.
Baada ya kukaa Shizuoka kwa raha, Anna na Sakura wanarudi Tokyo. Kenta yuko kwenye kituo cha treni kuwasindikiza.
-
Somo la 37: Niliona mlima Fuji, nikala sushi na kadhalika.
Anna amerejea bwenini jijini Tokyo kutoka mji wa Shizuoka. Anamueleza mama msimamizi wa bweni jinsi safari yake ilivyokuwa.
-
Somo la 38: Sawa.
Anna alipoamka asubuhi, alihisi uchovu na homa. Anakwenda hospitalini pamoja na Mama msimamizi wa bweni.
-
Somo la 39: Nafikiri una homa.
Anna hahisi vizuri, na amekwenda hospitalini, akiwa ameambatana na mama msimamizi wa bweni. Sasa anamwona daktari.
-
Somo la 40: Kichwa kinauma.
Anna amepata homa na amelala chumbani mwake. Mama msimamizi wa bweni ana wasiwasi na amekwenda kumuangalia anavyoendelea.
-
Somo la 41: Nilifurahi kwa kuwa niliweza kwenda kwenye tamasha la chuoni.
Anna amepona homa. Leo anaandika barua pepe kwa Kenta, ambaye alimtembeza mjini Shizuoka.
-
Somo la 42: Sijui kipi ni kitamu zaidi?
Anna yupo kwenye ziara ya kimasomo. Ananunua kasha la vyakula kwenye treni ya mwendo kasi ya Shinkansen.
-
Somo la 43: Unadhani ni kwa nini?
Anna yupo katika ziara ya kimasomo. Leo amekwenda kwenye kasri la Himeji mkoani Hyôgo.
-
Somo la 44: Baada ya kula vitamutamu vya Kijapani, unakunywa chai ya kijani.
Baada ya kutembelea kasri la Himeji, Anna amehudhuria hafla ya chai kwenye nyumba iliyo karibu ambapo hafla hiyo hufanyika.
-
Somo la 45: Kheri ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa!
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya Anna. Rafiki zake wanasherehekea siku hiyo mgahawani.
-
Somo la 46: Nimefurahi kuona theluji, kabla ya kurejea nchini kwangu
Baada ya kusherehekea kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya Anna, Kenta alijitolea kumrejesha bwenini. Walipotoka, theluji ikaanza kudondoka.
-
Somo la 47: Ndoto yangu ni kuwa mwalimu wa lugha ya Kijapani
Muda wa masomo wa Anna wa takriban mwaka mzima nchini Japani, umekaribia kukamilika. Leo Anna atakuwa na darasa la mwisho katika chuo kikuu.
-
Somo la 48: Asante kwa yote
Leo, Anna anarejea nchini Thailand. Sakura na Kenta wamekwenda uwanja wa ndege kumuaga.