NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 11

Somo la 11

Tafadhali fanya kila namna ufike.

Karamu itafanyika katika bweni ambalo wanafunzi wa kigeni wanaishi akiwemo Anna. Anna anamkaribisha Sakura kwenye karamu.

Somo la 11 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

ZEHI KITE KUDASAI

Mazungumzo

アンナ 今週の土曜日に寮でパーティーを開きます。
さくらさん、ぜひ来てください。
Jumamosi wiki hii, tutakuwa na karamu katika bweni letu.
Sakura, tafadhali fanya kila namna ufike.
Anna KONSHÛ NO DOYÔBI NI RYÔ DE PÂTÎ O HIRAKIMASU.
SAKURA-SAN, ZEHI KITE KUDASAI.
Jumamosi wiki hii, tutakuwa na karamu katika bweni letu.
Sakura, tafadhali fanya kila namna ufike.
さくら わあ、行く行く。
今度の土曜日ね。
Oh, ningependa kwenda. Jumamosi hii, au siyo?
Sakura WÂ, IKU IKU.
KONDO NO DOYÔBI NE.
Oh, ningependa kwenda. Jumamosi hii, au siyo?

Vidokezo vya sarufi

Siku za wiki

Ili kujifunza namna ya kutaja siku za wiki, tafadhali angalia "Nyenzo za kujifunzia."

IKIMASU na KIMASU

Kwa Kijapani, unatumia kitenzi tofauti kulingana na mtazamo wa mzungumzaji.

Mwalimu Tufundishe

Vitenzi vya umbo la kikamusi
Kamusi za Kijapani zinaorodhesha vitenzi katika umbo hili. Ikiwa utatumia umbo hili, utasikika katika hali ya kawaida zaidi.

Tanakali Sauti

Uchangamfu
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Sakura alisema atakuja karamuni. UKI UKI.
Je, atapenda chakula cha asili ya Thailand nitakachopika? Ninahisi WAKU WAKU.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.