NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 33

Somo la 33

Anna, nitakupatia.

Anna amekwenda kwenye tamasha la chuo kikuu pamoja na Kenta ambaye ni binamu yake Sakura. Wanaangalia maonyesho ya picha yaliyoandaliwa na klabu ya upigaji picha.

Somo la 33 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

ANNA-SAN NI AGEMASU

Mazungumzo

健太 これは、僕が富士山で撮った写真です。 Hii ni picha niliyopiga nikiwa mlima Fuji.
Kenta KORE WA, BOKU GA FUJISAN DE TOTTA SHASHIN DESU.
Hii ni picha niliyopiga nikiwa mlima Fuji.
アンナ あっ、私だ。 Oh, yule ni mimi.
Anna A', WATASHI DA.
Oh, yule ni mimi.
健太 驚いた?
あとで、アンナさんにあげます。
Umeshangaa?
Anna, nitakupatia baadaye.
Kenta ODOROITA?
ATODE, ANNA-SAN NI AGEMASU.
Umeshangaa? Anna, nitakupatia baadaye.
アンナ 写真をくれるんですか。うれしいです。 Utanipatia picha? Nitafurahi.
Anna SHASHIN O KURERU N DESU KA? URESHII DESU.
Utanipatia picha? Nitafurahi.

Vidokezo vya sarufi

AGEMASU na KUREMASU

Katika Kijapani vitenzi tofauti hutumika, kutegemea mtazamo wa mtoaji au mpokeaji.
Wakati mzungumzaji anapompatia kitu msikilizaji, anasema  AGEMASU. Ikiwa mtu fulani atakupatia kitu, tumia neno KUREMASU.
Kwa kujifunza zaidi, tafadhali usome  kona ya "Mwalimu, tufundishe."

Mwalimu Tufundishe

Tofauti kati ya AGEMASU na KUREMASU
katika Kijapani vitenzi tofauti hutumika, kutegemea mtazamo wa mtoaji au mpokeaji.

Tanakali Sauti

Tabasamu
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Kwenye tamasha la chuoni, kulikuwa na vibanda vya vyakula. Nilikula tambi za kukaangwa, yakisoba. Inasemekana msimu wa pukutizi ni msimu wa sanaa, michezo na vilevile hamu ya kula. Kwa kweli huu ni msimu mzuri!

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.