Somo la 35
Naweza kutumia kadi ya kufanyia manunuzi?
Anna pamoja na Kenta, walifurahia mlo wa sushi katika mgahawa wenye mikanda ya kubebea chakula.
Usemi wa msingi:
KUREJITTO KÂDO WA TSUKAEMASU KA
Mazungumzo
健太 | お勘定をお願いします。 | Naweza kupata bili yangu, tafadhali?
|
---|---|---|
Kenta | OKANJÔ O ONEGAI SHIMASU.
Naweza kupata bili yangu, tafadhali?
|
|
店員 | 全部で5200円です。 | Kwa jumla, ni yeni 5,200.
|
Muuzaji | ZENBU DE GOSEN NIHYAKU EN DESU.
Kwa jumla, ni yeni 5,200.
|
|
健太 | クレジットカードは使えますか。 | Naweza kutumia kadi ya kufanyia manunuzi?
|
Kenta | KUREJITTO KÂDO WA TSUKAEMASU KA.
Naweza kutumia kadi ya kufanyia manunuzi?
|
|
店員 | はい、使えます。 | Ndiyo, unaweza kutumia.
|
Muuzaji | HAI, TSUKAEMASU.
Ndiyo, unaweza kutumia.
|
Vidokezo vya sarufi
Namba (3)
Tujifunze namba kubwa.
Tafadhali tembelea ukurasa wa nyezo za kujifunzia.
Mwalimu Tufundishe
Umbo la uwezekano la vitenzi
Umbo la uwezekano la vitenzi huwa na maana mbili.
Tanakali Sauti
Sauti za elektroni
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Kenta alinipeleka nikale sushi! Unasema GOCHISÔSAMA DESHITA baada ya kula. Pia nimejifunza ya kwamba unasema GOCHISÔSAMA DESHITA, kwa mtu aliyekulipia chakula.