Somo la 5
Hizo ni hazina zangu.
Anna amemwalika Sakura kwenye chumba chake bwenini. Sakura aliona kitu.
Usemi wa msingi:
SORE WA WATASHI NO TAKARAMONO DESU
Mazungumzo
アンナ | 私の部屋はこちらです。どうぞ。 | Chumba changu kiko upande huu. Karibu.
|
---|---|---|
Anna | WATASHI NO HEYA WA KOCHIRA DESU. DÔZO.
Chumba changu kiko upande huu. Karibu.
|
|
さくら | すごい!これは全部マンガ? | Inashangaza! Zote hizi ni katuni za manga?
|
Sakura | SUGOI! KORE WA ZENBU MANGA?
Inashangaza! Zote hizi ni katuni za manga?
|
|
アンナ | それは私の宝物です。 私は毎日マンガを読みます。 |
Hizo ni hazina zangu. Mimi huwa ninasoma katuni za manga kila siku. |
Anna | SORE WA WATASHI NO TAKARAMONO DESU. WATASHI WA MAINICHI MANGA O YOMIMASU. Hizo ni hazina zangu.
Mimi huwa ninasoma katuni za manga kila siku. |
Vidokezo vya sarufi
Kiima WA Mtendwa O Kitenzi
Mpangilio wa maneno kwa Kijapani ni "kiima, mtendwa, na kitenzi."
O inaonyesha mtendwa.
k.m.) WATASHI WA MANGA O YOMIMASU. (Ninasoma manga.)
Mwalimu Tufundishe
Namna ya kuweka kitenzi katika hali ya kukanusha na swali
Vitenzi vinavyoisha na MASU vinaitwa “vitenzi vya umbo la MASU.” Utatumia umbo la MASU, ikiwa unazungumza kiungwana. Ili tuigeuze ilete dhana ya kukanusha, tunageuza MASU iwe MASEN. Kwa hiyo, YOMIMASU (kusoma) inabadilika na kuwa YOMIMASEN.
Tanakali Sauti
Kusoma vitabu
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Pengine Sakura alifikiria mimi huwa ninasoma katuni za manga kila wakati bila kufanya jambo jingine. Lakini kwangu mimi, Manga ni nyenzo nzuri za kujifunza Kijapani.