NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 8

Somo la 8

Rudia tafadhali.

Anna anahudhuria somo la Kijapani linaloongozwa na Profesa Suzuki katika chuo kikuu.

Somo la 8 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

MÔICHIDO ONEGAI SHIMASU

Mazungumzo

先生 みなさん、これを覚えてください。
試験によく出ます。
Kila mmoja, tafadhali kumbuka hii. Mara nyingi hutokea kwenye mtihani.
Mwalimu MINASAN, KORE O OBOETE KUDASAI.
SHIKEN NI YOKU DEMASU.
Kila mmoja, tafadhali kumbuka hii. Mara nyingi hutokea kwenye mtihani.
学生 えっ。 Hee!
Wanafunzi E'.
Hee!
アンナ 先生、もう一度お願いします。 Mwalimu, rudia tafadhali.
Anna SENSEI, MÔICHIDO ONEGAI SHIMASU.
Mwalimu, rudia tafadhali.

Vidokezo vya sarufi

Vitenzi vya umbo la TE

Vitenzi vinapotumika katikati ya sentensi, yaani, unapoongeza maneno mengine baada ya vitenzi hivyo,  unatumia mnyambuliko wake.
Vitenzi vinavyonyambulika kumalizikia na TE au DE, huitwa "vitenzi vya umbo la TE.”

k.m.) OBOEMASU (kukumbuka) >> OBOETE

Tafadhali nenda kwenye "Nyenzo za kujifunzia."

Mwalimu Tufundishe

Kitenzi cha umbo la TE + KUDASAI
Kwa Kijapani unapomuomba mtu afanye kitu, unasema kwa kutumia vitenzi vya umbo la TE, kisha unaongeza KUDASAI (Tafadhali). Vitenzi vya umbo la TE ni vile vinavyonyambulika ambavyo vinaishia na TE au DE.

Tanakali Sauti

Mapigo ya moyo
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Kando na mtihani wa mwisho, nimesikia kutakuwa na majaribio. Ninahisi DOKI DOKI.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.