Nyenzo za kujifunzia
Namna ya kuunda vitenzi vya umbo la TE - Sehemu ya 2 (Somo la 9)
Tujifunze namna ya kuunda vitenzi vya umbo la TE kwa kuimba. Wimbo huu unakufahamisha vile unavyoweza kubadilisha vitenzi vya umbo la MASU hadi umbo la TE, ikitegemea na silabi zinazojitokeza kabla ya MASU. Imba wimbo huo na ukariri kanuni zinazotumika.I-CHI-RI TTE, MI-NI-BI NDE
I-CHI-RI TTE, MI-NI-BI NDE
KI ITE, GI IDE, ITTE
KI ITE, GI IDE, ITTE
Umbo la MASU | Umbo la TE |
---|---|
TSUKAIMASU (kutumia) |
TSUKATTE |
MACHIMASU (kusubiri) |
MATTE |
ATSUMARIMASU (kukusanyika) |
ATSUMATTE |
YOMIMASU (kusoma) |
YONDE |
KAKIMASU (kuandika) |
KAITE |
ISOGIMASU (kufanya haraka) |
ISOIDE |
IKIMASU (kwenda) |
ITTE |
Tuna maelezo ya kina kuhusu kinachoendelea katika masomo ya sauti. Tafadhali nenda kwenye ukurasa wa masomo kwa kubofya kitufe cha chini, na usikilize somo hilo la dakika 10 katika ukurasa huo.