Kifahamu Kijapan “Brokoli ni mboga muhimu kwa maisha ya watu wa Japani”

Karibu katika kipengele cha "Kifahamu Kijapani" ambapo utaweza kujifunza kuhusu nchi ya Japani pamoja na lugha ya Kijapani kupitia taarifa ya habari iliyosomwa kwa lugha rahisi ya Kijapani.
Kichwa cha Habari cha taarifa ya leo ni “Brokoli ni mboga muhimu kwa maisha ya watu wa Japani.” Hii ni taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya NEWS WEB EASY tarehe 24 mwezi Januari mwaka huu. Misamiati muhimu inajumwisha 「指定野菜(していやさい)shitee-yasai」“mboga zilizoteuliwa” na 「栄養(えいよう) eiyoo」“virurubisho.”

“Brokoli ni mboga muhimu kwa maisha ya watu wa Japani”




Karibu katika kipindi cha Kifahamu Kijapani, mimi ni Radhia Suzuki.

Jiunge nasi ili ufahamu mengi kuhusu nchi ya Japani na lugha ya Kijapani kupitia taarifa ya habari ya Kijapani.
Kichwa cha habari leo hii ni…



「ブロッコリーは日本(にっぽん)の人(ひと)たちの生活(せいかつ)に大切(たいせつ)な野菜(やさい)」

“Brokoli ni mboga muhimu kwa maisha ya watu wa Japani”
Taarifa hii imechapishwa katika tovuti ya NEWS WEB EASY tarehe 24 mwezi Januari mwaka huu.
Kwanza tupitie misamiati kadhaa itakayokusaidia kuelewa taarifa hii.

指定野菜(していやさい)
Msamiati huu unarejelea orodha ya wizara ya kilimo ya mboga muhimu zilizoteuliwa ambazo zinaliwa kwa wingi kote nchini Japani.

栄養(えいよう)
virurubisho

Tuzingatie misamiati hii tunaposikiliza taarifa kamili.

「国(くに)は、日本(にっぽん)の人(ひと)たちがよく食(た)べていて、生活(せいかつ)に特(とく)に大切(たいせつ)な野菜(やさい)を「指定野菜(していやさい)」にしています。今(いま)はキャベツ、だいこん、トマト、なす、ねぎ、たまねぎなど 14 の野菜(やさい)があります。
2026 年(ねん)からブロッコリーが新(あたら)しく指定野菜(していやさい)になります。日本(にっぽん)では人口(じんこう)が少(すく)なくなって、市場(いちば)に出(で)る野菜(やさい)の量(りょう)が少(すく)なくなっています。しかし、ブロッコリーは最近(さいきん)の 10 年(ねん)で 30%ぐらい増(ふ)えました。栄養(えいよう)が多(おお)いことなどが、よく食(た)べるようになった理由(りゆう)です。
指定野菜(していやさい)の値段(ねだん)が下(さ)がったときは、たくさん作(つく)っている農家(のうか)が仕事(しごと)を続(つづ)けることができるように、国(くに)がお金(かね)を出(だ)します。」

Ulaji wa mboga ya brokoli umekuwa ukiongezeka nchini Japani na serikali imeamua kujumuisha mboga hiyo katika orodha ya “mboga zilizoteuliwa” ambazo zinafikiriwa kuwa na ulazima katika maisha ya watu wanaoishi nchini humo.



Sasa nitafafanua baadhi ya sentensi katika taarifa hii ambazo zina semi na maneno muhimu. Tuanze na sentensi ifuatayo:

2026 年(ねん)からブロッコリーが新(あたら)しく指定野菜(していやさい)になります。

“Kuanzia mwaka 2026, mboga ya brokoli itakuwa mboga mpya kuteuliwa.”

Katika msamiati 指定野菜(していやさい), 指定(してい) ni nomino inayomaanisha “uteuzi.” Umbo la kitenzi ni 指定(してい)する, yaani “kuteua.” Katika muktadha wa taarifa hii, 指定(してい) inarejelea mamlaka ya serikali kutoa amri na kukipa kitu hadhi maalum.

Kwa hiyo mboga inapopewa hadhi ya 「指定野菜(していやさい)」 inamaanisha serikali inatambua umuhimu wake na itahakikisha upatikanaji thabiti.

Neno 「指定(してい)」 pia hutumika katika maisha ya kila siku kubainisha mtu, muda, mahala au kitu kwa ajili ya kazi ama kusudio maalum.
Kwa mfano, 時間(じかん)を指定(してい)する inamaanisha “kubainisha muda.” Mtu anapokupa maelekezo na kusema 指定(してい)された時間(じかん)に来(き)てください, anamaanisha, “tafadhali njoo kwa wakati uliopangwa.”

Pia utasikia neno hili katika masuala ya treni za mwendokasi na treni maalum za mwendokasi. Siti maalum zilizohifadiwa huitwa 指定席(していせき), wakati siti ambazo hazijahifadhiwa huitwa 自由席(じゆうせき).

Hadi sasa, Japani ina mboga 14 katika orodha yake ya「指定野菜(していやさい)」.

Bila shaka nitazitaja mboga hizo moja baada ya nyingine, tuone ni mboga ngapi unazozifahamu.

キャベツ、kabichi、きゅうり、matango、さといも、magimbi、だいこん、figili nyeupe、たまねぎ、vitunguu、 トマト、nyanya、なす、biringani、ねぎ、vitunguu kijani、にんじん、karoti、 はくさい、kabichi ya kichina、じゃがいも、viazi、 ピーマン、pilipili hoho、ほうれんそう、mchicha、 レタス、majani ya saladi.

Mboga ngapi ulizozitambua? Mboga hizi ni za kawaida sana nchini Japani, kwa hiyo huu ni wakati mwafaka kuzifahamu mboga hizi.

Sawa, tuendelee na sentensi ifuatayo.

指定野菜(していやさい)の値段(ねだん)が下(さ)がったときは、たくさん作(つく)っている農家(のうか)が仕事(しごと)を続(つづ)けることができるように、国(くに)がお金(かね)を出(だ)します。

“Bei ya mboga zilizoteuliwa inaposhuka, serikali hutoa fedha ili wakulima wanaozalisha mboga hizo kwa wingi waweze kuendelea kufanya kazi.”

Neno ように hutumika katika hali mbalimbali.
Hapa, linatumika kuelezea hali au matokeo yanayotarajiwa.

Inasema kwamba serikali inataka kuhakikisha wakulima waweze kuendelea kulima mboga zao.
Kinachofuata 「ように」ni hatua maalum itakayochukuliwa kuhakikisha jambo hilo linatokea. Katika taarifa hii, inasemwa kwamba serikali itatoa ruzuku.
Uzalishaji na bei za mboga vinaweza kuathirika sana na sababu za kimazingira kama vile hali ya hewa, kwa hiyo kutambuliwa kama「指定野菜(していやさい)」ni jambo zuri kwa wazalishaji wa mazao.

Kwa hiyo, ように inaelezea kuchukua hatua fulani ili kufikia lengo. Mfano mwingine utakuwa ni 忘(わす)れないようにメモしておきます. Yaani “Nitaandika maelezo ili nisisahau.”

Kwa leo tutamalizia hapa. Taarifa ya leo imesema kwamba kiasi cha mboga ya brokoli inayoliwa na Wajapani kimeongezeka kwa asilimia 30 katika miaka 10 iliyopita!

Imekuwa mboga kuu kutokana na kwamba ina vitamini na virutubisho vingine na ni mboga nzuri kutumia katika saladi na mikaango. Pia ni mwafaka kwa kutia katika visanduku vya chakula vya Bento kama chakula cha pembeni.

Asante kwa kuwa nasi, jiunge nasi tena wakati ujao!