Ripoti: Afro Dance

Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea ripoti kuhusu tukio la kucheza Afro Dance lililoandaliwa na African Kids Club inayoendeshwa na shirikia lisilo la kujipatia faida la Africa Japan Forum. Tukio hili lilifanyika Juni 29, 2024 jijini Tokyo, Japani.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!

Kipindi hiki kilitangazwa Julai 14.

Miongoni mwa waratibu wa tukio hilo.
Watoto wenye asili ya Kiafrika wakicheza Afro Dance.
Watoto walioshiriki tukio hilo wakichora picha.
Picha ya pamoja ya washiriki wa tukio hilo.