Rakugo: Simulizi inayotokana na hadithi inayoitwa "Momotarou"

Hiki ni kipindi kinachosimulia simulizi fupi za kusisimua na kuvutia mno nchini Japani. Simulizi yetu wakati huu inatokana na hadithi fupi inayoitwa "Momotarou", mvulana wa pichi.

Momotarou ni simulizi maarufu sana ya kale nchini Japani, na simulizi yetu ya Rakugo inatokana na hadithi hii ya kale. Ni simulizi inayoangazia hadithi wanazosimuliwa watoto wanapotayarishwa kwenda kulala. Inahusisha Baba na Mwanawe wa kiume aitwaye Kenbou. Katika hadithi hii, Baba anamsimulia Kenbou kuhusu mwanamume mzee na mwanamke mzee walioishi hapo zamani za kale. Wawili hao walikuwa wanandoa wazuri na waaminifu, ila hawakujaaliwa mtoto. Siku moja, mwanamume mzee alienda mlimani kuchanja kuni, na mwanamke mzee alienda mtoni kuosha nguo. Alipokuwa akiosha nguo, mwanamke huyo aliona pichi kubwa likiogelea kumwelekea. Kisha alipolikata pichi lile katika vipande viwili kwa kutumia kisu, mtoto mvulana alichomoza kutoka ndani ya pichi!

Usikose kusikiliza simulizi hii kwa uhondo kamili. Aidha, watangazaji wetu nao watazamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukiwa umevunjika mbavu.

(Kipindi hiki kilitangazwa mnamo Mai 12, 2024.)