Ripoti: Waswahili No Kai

Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu tunakuletea ripoti kuhusu mkutano wa kundi la Wajapani waliofanya na wanaofanya kazi za kujitolea nchini Tanzania (Waswahili No Kai) na Balozi wa Tanzania nchini Japani Baraka Luvanda uliofanyika Machi 9, 2024 katika ubalozi wa Tanzania nchini Japani uliopo jijini Tokyo.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!

Picha ya pamoja ya Wajapani waliofanya na wanaofanya kazi za kujitolea nchini Tanzania (Waswahili) na Balozi wa Tanzania nchini Japani Baraka Luvanda.
Kiongozi wa Wajapani waliofanya na wanaofanya kazi za kujitolea nchini Tanzania (Waswahili) akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Japani Baraka Luvanda.
Mmoja wa Wajapani waliofanya kazi za kujitolea nchini Tanzania akikabidhi zawadi kwa balozi wa Tanzania nchini Japani Baraka Luvanda.
Mkutano wa Wajapani waliofanya na wanaofanya kazi za kujitolea nchini Tanzania (Waswahili No Kai) ulivyokuwa ukiendelea katika ubalozi wa Tanzania nchini Japani.