Kipindi: Semi za Kijapani

Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea Semi za Kijapani ambapo utapata mwanya wa kutanabahi misemo ya Kijapani na maana na matumizi yake, lakini pia kupitia kipindi hiki utaweza kujifunza lugha ya Kijapani pamoja na kukutana na maneno yanayofanana na yale ya Kiswahili.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!

(Kipindi hiki kilitangazwa Januari 21, 2024.)