Ripoti: Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Kenya

Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea ripoti kuhusu Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Kenya pamoja na Miaka 60 ya Uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Kenya na Japani yaliyofanyika ukumbi wa Conrad jijini Tokyo mnamo Desemba 12 mwaka 2023.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
(Kipindi hiki kilitangazwa Desemba 24, 2023.)

Keki maalumu ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Kenya.
Balozi wa Kenya nchini Japani, Tabu Irina akitoa hotuba katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Kenya, na Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Kenya na Japani.
Balozi wa Kenya nchini Japani, Tabu Irina akitoa hotuba katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Kenya, na Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Kenya na Japani.
Mwanadiaspora wa Kenya, Dick Olango akizungumzia Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Kenya wakati wa mahojiano na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya NHK WOLRD JAPAN, Mbozi Katala.