Ripoti: Tamasha la Siku ya Kiswahili Duniani

Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea ripoti kuhusu Tamasha la Siku ya Kiswahili Duniani lililofanyika katika ubalozi wa Tanzania nchini Japani uliopo jijini Tokyo.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
(Kipindi hiki kilitangazwa Julai 9, 2023.)

Matukio mbalimbali katika Tamasha la Siku ya Kiswahili Duniani.
Matukio mbalimbali katika Tamasha la Siku ya Kiswahili Duniani.
Matukio mbalimbali katika Tamasha la Siku ya Kiswahili Duniani.