Mahojiano: Mhandisi Florian Kalemera

Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea mahojiano na Mhandisi Florian Kalemera kutoka Wizara ya Kilimo nchini Tanzania kuhusiana na mkutano ulioandaliwa na kituo cha AFICAT, kupitia Shirika la Japani la Ushirikiano wa Kimataifa au JICA kuhusiana na matumizi ya mashine katika kilimo, uliofanyika katika hoteli ya New Otani iliyopo jijini Tokyo, Japani.
Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!

Mhandisi Florian Kalemera kutoka Wizara ya Kilimo nchini Tanzania akiwasilisha mada katika mkutano wa AFICAT.