Ripoti: Uchaguzi wa viongozi wa Tanzanite Society

Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu tunakuletea ripoti kuhusu uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Japani maarufu "TANZANITE SOCIETY" uliofanyika katika ubalozi wa Tanzania nchini Japani uliopo jijini Tokyo.

Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!