Sarafu za Dhahabu - Koban

Miaka 60 iliyopita, aina 3 za sarafu ya dhahabu za karne za 17 na 18 ziligunduliwa kwenye eneo la ujenzi katikati ya jiji la Tokyo. Zilikuwa ni sarafu za dhahabu (koban) zilizotumika kuanzia enzi ya Edo. Mng'ao wa dhahabu ulidumishwa kwa karne kadhaa na kuonyesha juhudi za serikali wakati huo kwa ajili ya kudumisha imani ya wananchi katika utumiaji wa sarafu hizo.

Sarafu ya dhahabu ya Keicho, sarafu ya dhahabu ya Shotoku, sarafu ya dhabu ya Kyoho