Fugen Bosatsu (Samantabhadra Bodhisattva)
(Fugen Bosatsu zo)

Mchoro wa karne ya 12, ni moja ya kazi bora za Kijapani katika imani ya kibuddha. Picha hiyo inaonyeshwa kwa Lotus Sutra, maandiko ya Kibuddha ambayo yalichukuliwa kuwa matakatifu nchini Japani kipindi hicho. Huku maua yakionyeshwa kwa rangi za kupendeza yakiwa yanapukutika kutoka juu, huu ni wakati ambao Fugen Bosatsu –Samantabhadra Bodhisattva ilipoanza kutambulika kwa wenye imani hiyo kutoka eneo la mbali la mashariki lililochukuliwa kuwa takatifu, akiwa amepanda ndovu mwenye rangi nyeupe na pembe sita. Mchoro huo una urefu wa sentimita 158.8 kwa upana wa 74.8, na kuchorwa kwenye kitambaa cha ya hariri kwa rangi za madini, dhahabu na fedha. Mapambo hayo yanaoneshwa kwa mbinu ya kirikane – ambapo ni mistari miembamba sana ya vipande vya dhahabu na kupachikwa kwenye kitambaa kwa kutumia gundi – yanavutia kupita kiasi. Mchoro huo unaashiria pendeleo la watu wa tabaka la juu wakati ambapo kwa kiasi kikubwa maisha yalikuwa yakizungukwa na siasa na utamaduni, japo kulikuwa na sababu zingine vilevile zilizochangia utengenezaji wa kazi nzuri kama hii.