Haniwa (sanamu ya makaburini) Iliyovalishwa mavazi ya kivita
(Haniwa, Keiko no bujin)

Haniwa ni sanamu ya terakota yaani iliyotengenezwa kwa udongo mwekundu mgumu, yenye rangi ya kahawia ambayo ina wekundu na vilevile ina nafasi. Hupatikana kwenye matuta ya makaburi ya viongozi wa maeneo husika ambayo yalijengwa nchini Japani kuanzia karne ya 3 hadi 6 baada ya kristo. Sanamu za Haniwa zilitengezwa kwa muundo mbalimbali kuanzia nyumba hadi watu na zilipangwa kwa safu ama kwa juu au mzunguko kwenye mpaka wa kaburi. Sanamu ya mpiganaji aliyevalia nguo ya vita ya Keiko, bado inapatikana hadi hii leo kutoka karne ya 6 tangu ilipofukuliwa mkoani Gunma mashariki mwa Japani. Mavazi na silaha za vita zimechongwa kwa usahihi na unaweza kuona vile wapiganaji wa wakati huo walikuwa wakivaa. Kati ya sanamu nyingi za Haniwa, hii ndiyo pekee iliyotambulika kama hazina ya Taifa. Picha yake zinaonekana kwenye stampu za posta na kama modeli ya mashujaa, katuni na filamu. Kwa nini wajapani wa zamani walikuwa wakichonga sanamu za Haniwa na kuziweka kwenye matuta ya makaburini? Ni nani aliyekuwa mpiganaji aliyevalia nguo ya vita ya keiko? Tutaangazia simulizi ya sanamu hiyo ya Haniwa ambayo bado inavutia katika Japani ya sasa.