Bakuli la kahawia linalokaa lenye kitako, ikiwa na kaa aliyepachikwa pembeni
Kazi ya Miyagawa Kouzan I
(Katsuyu Kani haritsuke Daitsuki Hachi)

Kaa wawili waliopachikwa pembeni mwa bakuli la kauri lililochongwa na kupakwa mng`ao wa rangi ya kahawia. Kila kitu kuhusu kaa hao kina uhalisia lakini pia ni sehemu ya bakuli hilo. Lilitengenezwa na Miyagawa Kouzan, msanii wa ufinyanzi ambaye jina lake lilivuma sana alipokuwa Kyoto akiwa na umri mdogo na baadaye akahamia Yokohama. Bidhaa za kauri zilikuwa ni moja ya bidhaa kutoka Japani zinazouzwa nje ya nchi katika kipindi cha mwishoni mwa nusu ya karne ya 19 na wabunifu walihitajika kuboresha ujuzi kadiri ya uwezo wao ili kutengeneza bidhaa ambazo zingevutia dunia. Hayo yalijitokeza wazi katika maonyesho makubwa yaliyofanyika kwenye nchi za magharibi. Sifa za Kouzan zilitokana na ubunifu wake wa hali ya juu wa mapambo ya kwenye michongo mfano wa sanamu iliyochongwa kwa kutokeza katika msingi wake maarufu kama “takaukibori” kwa Kijapani, ikiwa ni pamoja na kaa wanaoonekana hapa. Hii ni simulizi ya fundi-stadi aliyetunukiwa heshima ya Taifa kwa misingi ya utamaduni na hali ya kisasa, Japani na duniani kwa ujumla.