Upanga, kazi ya Masamune ambayo haijatiwa saini (maarufu kama Kanze Masamune)
(Katana mumei Masamune, meibutsu Kanze Masamune)

Upanga mrefu, mwembamba uliopinda kidogo. Japani ina utamaduni wa kufurahia upanga ukiwa umetolewa kwenye ala zake za mapambo, na mapambo mengine. Tunu hii ya taifa, Upanga wa Masamune usiotiwa saini, ulitengenezwa katika karne ya kumi na nne na Masamune, mmoja ya wahunzi mashuhuri zaidi wa zama za utengenezaji upanga. Tukiangalia kwa karibu upanga huo, tunaona mitindo ya urembo ya vitu vinavyong’aa na mitindo mbali mbali kwenye sura ya chuma cha pua inayofanana na vifundo kwenye mbao. Mitindo hii inatokana na mchakato wa kutengeneza chuma ili kutengeneza upanga ulio imara na wakati huo huo wenye uwezo wa kunesa nesa. Panga za Masamune zinathaminiwa mno kwa mvuto wake kwenye sehemu yenye makali. Masamune, na ustadi wake wa utengenezaji upanga wa enzi hizo, bado hafahamiki. Umiliki wa upanga wa Masamune ulifikia hadi ukaonekana kama hadhi ya juu zaidi kwa watu wa tabaka la watawala. Kama zawadi, panga hizo zilitumika kama ishara ya taadhima ya samurai na kubadilisha umiliki wake mara kwa mara.