Dogu yenye miwani ya jua iliyopatikana katika eneo la kihistoria la Kamegaoka mkoani Aomori
(Shakouki Dogu)

Dogu au kinyago cha ufinyanzi iliyochomwa kwenye tanuru ya moto ambayo inadhaniwa ilitengenezwa kati ya miaka 2,500 na 3,000 iliyopita. Mabadiliko ya umbo lake la mwili, macho makubwa na ubunifu wa kina, ni sifa za kipekee. Jina la "Dogu yenye miwani" lilitumika kwa sababu inaonekana kama mtu aliyevaa miwani ya jua inayofanana na ile iliyovaliwa na watu wa asili ya Canada wanaoishi pwani ya kaskazini, kwa ajili ya kujikinga na mwanga wa theluji. Haijulikani ufinyanzi huo ulibuniwa kwa ajili gani, lakini kukosekana kwa kipande cha mguu mmojawapo kunaweza kutoa dondoo. Baadhi ya wataalamu wanasema, iliharibiwa kwa makusudi ili kujitoa kama sadaka, ili kwamba watu wasiweze kupata majeraha na majanga. Tutaangazia kwa karibu ufinyanzi huo wenye kuhusishwa na maombi ya watu wa zamani.