Somo la 48: Nikihitimu, nataka kufanya kazi nchini Japani.

Wakazi wa "Nyumba ya Haru-san" wapo ziarani Kyoto. Wamefika kwenye moja ya mahekalu maarufu ya Kyoto, Kiyomizu-dera. Tam anafichua ndoto yake wakiwa wamesimama kwenye jukwaa la ukumbi mkuu. Katika somo hili, utajifunza namna ya kusema tunachotaka kufanya siku za usoni. Baadaye katika kipindi, tutazungumzia vyakula vya maeneo.

Pia tuna ukurasa wa tovuti uliosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemsha bongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.

Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.