Somo la 46: Ni ndogo lakini inapendeza.

Ni takribani mwaka mmoja tangu Tam alipowasili Japani kutokea Vietnam. Wakazi wote wa "Nyumba ya Haru-san" wameenda ziarani Kyoto. Wanakaribia kujiandikisha katika hoteli inayotumia "machiya." Machiya ni nyumba za mbao za mjini zinazojipanga kwenye mitaa myembamba. Katika somo hili, utajifunza namna ya kuelezea fikra mbalimbali baada ya kujifunza somo la 26. Baadaye kwenye kipindi, tutazungumzia uzuri wa Kyoto.

Pia tuna tovuti iliyosheheni nyenzo za kukusaidia kujifunza Kijapani kama vile sauti, maandishi, katuni ya anime ya mazungumzo ya somo, chemshabongo na kadhalika. Bofya tu linki iliyo chini ya picha.

Ili kutembelea tovuti ya Jifunze Kijapani, bofya hapa.