#29 Nilikwenda kusikiliza onyesho la piano.

Ili kuelezea kwa nini ulienda sehemu fulani, badili "masu" kwenye kitenzi mfano "kikimasu" (kusikiliza) kwa kuweka "ni ikimashita" (-likwenda kufanya kitu). "Piano no ensoo o kiki ni ikimashita" inamaanisha "Nilikwenda kusikiliza onyesho la piano."

Transcript