Biringani
Kipindi cha "Vinono kutoka jijini Tokyo" kinaangazia vyakula mbalimbali vinavyopatikana kwenye masoko ya jiji hilo likiwemo soko la Toyosu. Wakati huu, tunaangazia biringani, linalojulikana kwa Kijapani kama "nasu", mbogamboga muhimu katika chakula cha Kijapani. Miaka iliyopita, Japani imeendeleza idadi kubwa ya mabiringani ya maeneo, kila aina ikiendana na hali ya hewa ya eneo husika. Niigata ni mkoa unaojulikana kama mmoja wa vinara wa uzalishaji mpunga Japani. Isitoshe, eneo la uzalishaji wa biringani mkoani humo ndilo kubwa zaidi Japani. Tunatembelea mkoa wa Niigata na kuona namna Wajapani wanavyopenda mbogamboga hiyo.
Kuna aina mbalimbali za mabiringani katika soko la Toyosu.
Mabiringani ya Yaki-nasu yanaweza kukua hadi ukubwa wa karibu sentimita 30, juu kidogo ya ardhi.
Biringani la Kijani, Sasakami-nasu ni adimu na lenye thamani sana.
Wakulima wanapenda vyakula vyenye aina mbalimbali za mabiringani.