Yamaimo
"Vinono kutoka jijini Tokyo" hukutambulisha vyakula mbalimbali vipatikanavyo kwenye masoko jijini Tokyo yakiwemo Tsukiji, lililojulikana kama "jiko la Tokyo," kwa miaka mingi pamoja na Toyosu, mrithi wake. Katika kipindi hiki, tunaangazia "yamaimo" viazi vya milimani vya Kijapani. Viazi hivyo huwa na ladha na ulaini wa viwango mbalimbali kulingana na vilivyopikwa. Tunazuru mgahawa wa karne unaotayarisha chakula cha kitamaduni cha viazi hivyo. Pia tutafahamu namna viazi hivyo vinavyogeuka kuwa vitamutamu vya Kijapani. (Kipindi hiki kilitangazwa Novemba 16, 2018.)
Viazi vya milimani vya Kijapani huja katika ukubwa na maumbo mbalimbali.
Mkulima wa viazi Kazuyoshi Sunaga (kushoto) na ripota Janni Olsson.
Viazi hutengenezewa okonomiyaki, chakula mfano wa chapati laini.
Vitamutamu vya Kijapani vilivyotengenezwa kulingana na misimu ya mwaka.