Kanpyo
Kipindi cha "Vinono kutoka jijini Tokyo" kinaangazia vyakula mbalimbali vinavyopatikana kwenye masoko ya jiji hilo ikiwa pamoja na soko la Toyosu. Wakati huu tunaangazia kanpyo, chakula kilichochakatwa kilichovumbuliwa Japani. Kina mwonekano wa tambi nyeupe za nudo zilizo bapa na huchemshwa pamoja na sosi ya soya na sukari ili kutumika katika miviringisho ya sushi. Tunakujuza mhimili uliojificha wa chakula cha Kijapani, kanpyo. (Kipindi hiki kilitangazwa 5 Agosti, 2020.)
Wakulima huleta vibuyu ndani na kuvining'iniza kwenye fito ili vikauke.
Ripota wa NHK WORLD-JAPAN Saskia Thoelen amtembelea muuzaji wa jumla wa vyakula vilivyokaushwa.
Kibuyu kinachongwa hadi unene wa milimita tatu ili kutengeneza kanpyo.
Nyama choma ya tochigi yenye kanpyo na vipande vya kitunguu.