Limao
Kipindi cha "Vinono kutoka jiji la Tokyo" kinakutambulisha vyakula mbalimbali vinavyopatikana katika masoko ya jijini humo ikiwa ni pamoja na Tsukiji, ambalo kwa miaka mingi lilikuwa likifahamika kama "Jiko la Tokyo," na Toyosu, mrithi wake. Kipindi hiki kitahusiana na limao, tunda jamii ya chungwa kama vile yuzu na mikan. Mkoa wa Hiroshima ni mzalishaji mkubwa wa malimao kuliko sehemu yoyote Japani. Tutaangalia namna watu huko wanavyohudumia matunda hayo na kutumia limao katika mapishi yao. (Kipindi hiki kilitangazwa Machi 27, 2020.)
Aina mbalimbali ya malimao yanaweza kupatikana katika soko la Toyosu.
Ripota wa NHK WORLD-JAPAN Kailene Falls akisaidia kuvuna.
Wakulima wa malimao katika eneo hilo wanafanya kazi kuboresha udongo wa asili.
Mbogamboga zilizokaangwa na limao