Viazi vitamu vilivyokaushwa vyatengenezwa nchini Tanzania kulenga soko la Japani
"Hoshiimo," viazi vitamu vilivyokaushwa ni chakula cha jadi cha Kijapani. Mjasiriamali Mjapani aliyeona umashuhuri wake nchini Japani, anavizalisha Tanzania nchi ambayo ni mzalishaji mkubwa wa viazi vitamu duniani.
Viazi vitamu vilivyokaushwa au "Hoshiimo" kwa Kijapani, ni chakula cha jadi cha Kijapani ambacho hutengenezwa kwa kuchemshwa, kukatwa na kukaushwa.
Pendekezo jipya la namna ya kula lililotolewa katika hoteli moja ya mkoa wa Ibaraki ulio mashuhuri kwa uzalishaji wa Hoshiimo, linavutia nadhari kutoka vijana.
Hasegawa Tatsuo, mjasiriamali Mjapani anashirikiana na wakulima wa Tanzania kulima viazi vitamu vya ubora wa hali ya juu.
Hasegawa amefaulu kutengeneza Hoshiimo kwa kutumia viazi hivyo pamoja na wafanyakazi wenyeji.