Semina ya "Africa Hack Collabo" 2
Semina iliyojulikana kama Africa Hack Collabo ilifanyika mwishoni mwa mwezi Agosti jijini Tokyo kwa lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara wa Japani na wale wa Afrika. Utasikiliza mahojiano na baadhi ya wawakilishi kutoka makampuni na idara za serikali za Afrika kuhusu malengo yao kuja kwenye semina hii nchini Japani.