Jishin, Kaminari, Kaji, Oyaji
Kipindi cha Semi za Kijapani kinakupa mwanya wa kutanabahi misemo ya Kijapani, maana na matumizi yake, huku kujifunza lugha na tamaduni za Japani sambamba na kukutana na misemo na maneno yanayofanana na yale ya Kiswahili.
Safari hii tutajifunza semi hii, "Jishin, Kaminari, Kaji, Oyaji." Tafsiri ya neno kwa neno ni "Tetemeko la ardhi, Radi, Moto, Baba." Je, inamaanisha nini? Mwalimu Kadoya Masaaki ndiye anayetuongoza darasani. (Kipindi hiki kimetangazwa Jumapili.)