Kazini nchini Japani ni kipindi kinachoangazia maisha ya raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Japani. Katika kipindi hiki, tunakusogeza karibu na tukio moja jijini Tokyo ili kumwangalia mzaliwa wa Uingereza Chris Peters akifanya tumbuizo. (Kipindi hiki kilitangazwa Machi 2, 2023.)
Chris mwenye umri wa miaka hamsini na moja yuko nchini Japani lakini amekuwa akifanya maonyesho mbalimbali duniani kote.
Hajawahi kukosa sanduku lake analoliamini lililojazwa na kila aina ya vifaa vya maonyesho.
Chris alitembelea Japani mnamo mwaka 1998 na kukutana na mshirika wake wa Kijapani K-Bow (kushoto). Waliunda kundi linaloitwa Funny Bones mnamo mwaka 2002.
Rekodi yao mahususi inayopendwa na watu ni "Bwana Dubwana" ambayo ni mchezo wa kuigiza. Chris na K-Bow kila mmoja huvaa aina ya "vazi la kikaragosi", na kuwageuza kuwa kama pandikizi la "Bwana Dubwana."