Tambi Huwaleta Watu Pamoja
Kazini nchini Japani ni kipindi kinachoangazia maisha ya raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Japani. Katika kipindi hiki, tumetembelea duka la tambi za soba mjini Zushi mkoani Kanagawa, linaloendeshwa na mzaliwa wa Bangladesh Muhammad Rezaul Karim Chowdhury.
Chowdhury kwa mara ya kwanza alikuja nchini Japani kama mwanafunzi mwaka 1993. Alipojaribu tambi za soba kwa mara ya kwanza, mara moja alipenda ladha ya kawaida ya tambi hizo.
Chowdhury anasisitiza katika kuhudumia tambi za soba zilizotoka kuandaliwa wakati huo, kukatwa wakati huo na kuchemshwa wakati huo.
Kutsuma Hiroyuki (kushoto) ni rais wa kiwanda cha ngano. Alivutiwa na shauku ya Chowdhury na kisha kumfundisha namna ya kutengeneza tambi za soba.
Chowdhury ameweka ubalaza katika paa la mgahawa wake. Ubalaza huo unaonyesha mwonekano mzuri wa mji wa Zushi, eneo la wazi la ubalaza huo limejazwa na tabasamu la wateja.