Kuelekea Ustadi wa Sushi
Kazini nchini Japani ni kipindi kinachoangazia maisha ya raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Japani. Katika kipindi hiki, tumetembelea mgahawa wa sushi jijini Tokyo ambapo mzaliwa wa China Wen Shuqi anapata mafunzo ya kuwa mpishi wa sushi. (Kipindi hiki kilitangzwa Januari 5, 2023.)
Wen Shuqi mwenye umri wa miaka 27, amekuwa akifanya kazi katika mgahawa uliopo Ginza jijini Tokyo tangu mwaka 2019.
Sushi ya Shuqi iliyowekewa juu samaki aina ya gizzard shad.
Akinuia kuwa mpishi kamili wa sushi, Shuqi anajifunza namna ya kuandaa sushi kutoka kwa mpishi mkuu na meneja wa mgahawa huo, Murayama Daisaku, baada ya mgahawa kufungwa.