Ndoto ya Kilimo ya Raia wa Indonesia mkoani Gunma
Kazini nchini Japani ni kipindi kinachoangazia maisha ya raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Japani. Katika kipindi hiki, tunatembelea shamba lililopo mkoa wa Gunma ambapo raia wa Indonesia Miko Alasta anasimamia kilimo cha letasi na uvunaji wa stroberi.
Miko Alasta mwenye umri wa miaka 25 amekuwa akifanya kazi katika shamba lililopo kijiji cha Showa mkoani Gunma tangu mwaka 2016.
Stroberi zinazolimwa katika shamba hilo ni za aina ya Yayoi Hime, zinazopendwa kwa mchanganyiko wake ulio sawia wa ladha tamu na chachu.
Baada ya kujifunza nchini Japani, Miko ana ndoto ya kufungua duka la vifaa vya kilimo katika ardhi yake ya nyumbani.
Msimamizi Inaba Hisanori (kulia) amekuwa akimuona Miko akipata ujuzi na maarifa.