Kuhakikisha Taa za Kitamuduni Zinaendelea Kuwaka
Kazini nchini Japani ni kipindi kinachoangazia maisha ya raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Japani. Katika kipindi hiki, "tunakueleza kwa kina" kuhusu kazi ya mzaliwa wa Ufaransa Jeff Rudge, ambaye anatengeneza taa za karatasi za kitamaduni za Kijapani mkoani Ibaraki.
Jeff Rudge mwenye umri wa miaka 43, amekuwa akifanya kazi ya ufundi stadi wa taa za karatasi za Kijapani kwa kutumia karatasi za chochin tangu mnamo mwaka 2017.
Akitumia zana maalum, Jeff hupasua mwanzi mkavu wenye urefu wa mita tatu katika vipande kumi na moja.
Ili kutengeneza umbo la taa, Jeff huvipachika vipande vya mwanzi katika fremu ya mbao na kuviunganisha na kifaa cha mviringo chenye nyuzi.
Baba mkwe wa Jeff, ambaye ni mwalimu wake Iijima Minoru (kushoto). Minoru mwenye umri wa miaka 83 amekuwa akitengeneza taa kwa takribani miaka 50.