Kuweka Nguvu ya Asili kwenye Karatasi
Kazini nchini Japani ni kipindi kinachoangazia maisha ya raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Japani. Katika kipindi hiki, tumetembelea mkoa wa Kochi, ambapo mzaliwa wa Uholanzi Rogier Uitenboogaart anatengeneza karatasi za kitamaduni za Kijapani, au "washi."
Rogier Uitenboogaart alikuja Japani mara ya kwanza mwaka 1980. Anatumia njia ya kitamaduni na rafiki kwa mazingira kutengeneza "washi."
Rogier anatuonyesha baadhi ya "kozo," ambayo ni malighafi makuu yanayotumiwa kutengeneza "washi."