Kuitambua Ndoto nchini Japani na Kuifanikisha
Kazini Nchini Japani ni kipindi kinachoangazia maisha ya raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Japani. Katika kipindi hiki, tunakutana na mwanamke kutoka nchini Myanmar Nial Khan Cing maarufu kama Non Non ambaye alitambua ndoto yake ya kuwa mrembeshaji kucha akiwa nchini Japani na sasa ana saluni yake jijini Tokyo.
Non Non mwenye umri wa miaka hamsini na mbili amekuwa mrembeshaji kucha tangu mwaka 2012.
Non Non ambaye ni mrembeshaji kucha.
Kwa sasa, Non Non ana wateja wa mara kwa mara, wanaoenzi ujuzi na ukarimu wake.
Hasunuma Miyuki (kulia), anayetumia ofisi moja na Non Non, humtia moyo.