Kufikia Kilele cha Picha Zilizochapishwa kwa Kutumia Vibao Vilivyochongwa
Kipindi cha Kazini Nchini Japani, huangazia raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Japani.Wakati huu, tunatembelea karakana ya mzawa wa Canada David Bull iliyopo jijini Tokyo. David ni fundistadi ambaye pamoja na timu ya wenzake, wanatengeneza picha zilizochapishwa kwa kutumia vibao vilivyochongwa kwa kutumia mbinu iliyoheshimika kwa muda mrefu. (Kipindi hiki kilitangazwa Juni 30, 2022.)
David Bull mwenye umri wa miaka sabini ni mtengenezaji wa picha zilizochapishwa kwa kutumia vibao vilivyochongwa. Alivutiwa na picha hizo za Kijapani na kuamua kujitolea kuzitengeneza maisha yake yote.
Karakana ya David inatengeneza picha halisi kwa kutumia vibao.
Kwa kutumia patasi za aina mbalimbali, David huchonga vibao vya kuchapisha picha hizo.
Ishikawa Yoko (kushoto), mchapishaji, akielezea David anavyopenda kazi yake na amekuwa akifanya kazi naye kwa muda wa miaka kumi.