Kurithi Umahiri wa Kutengeneza Wagashi
Kazini Nchini Japani ni kipindi kinachoangazia maisha ya raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Japani. Katika kipindi hiki, tunakutana na Bill Leon Guerrero kutoka Guam ambaye ni mtengeneza vitamutamu vya Kijapani vinavyojulikana kama wagashi mkoani Ehime magharibi mwa Japani.
Bill Leon Guerrero mwenye umri wa miaka 61 amekuwa akitengeneza wagashi mkoani Ehime kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Daifuku halisi iliyotengenezwa na Bill. Daifuku na rojo ya maharagwe mekundu yaliyowekwa sukari na kisha kuzungushiwa kwenye tabaka la keki laini ya mchele.
Kiwanda cha Bill kinatengeneza karibu daifuku 1,800 kwa siku.
Mkewe Bill, Masuda Toshie (kulia) anamsaidia mumewe kazini. Mwanao wa kiume, Masuda Hiroki (katikati) ni mtengenezaji vitamutamu wa kizazi cha tatu.