Kupania kuwa Mpishi Mkuu wa Tambi za Rameni Nchini Japani
Kazini Nchini Japani ni kipindi kinachoangazia maisha ya raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Japani. Wakati huu, tunatembelea mgahawa wa Tran Van Trung ambaye ni mzawa wa Vietnam uliopo jijini Tokyo ili kufahamu mengi kuhusu tambi zake za rameni za supu ya samaki. (Kipindi hiki kilitangazwa Mei 5, 2022.)
Tran Van Trung alifungua mgahawa wake wa tambi za rameni 2017, na kutokana na supu yake iliyotengenezwa kwa njia maalum, mgahawa huo umekuwa maarufu kiasi kwamba wateja hupanga foleni nje.
Trung anatengeneza supu ya samaki akitumia jumla ya aina tano tofauti za samaki wa kukaushwa zilizochaguliwa kwa uangalifu kutoka kote Japani.
Tambi maalum za rameni za Trung ziko tayari.
Mkewe Trung, Chuyen (kulia) amekuwa akiunga mkono "Ndoto ya Kijapani" ya mumewe katika maisha yao ya kila siku na kazini.