Kukuza na Kutunza Misitu
Kazini nchini Japani huangazia maisha ya raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Japani. Katika kipindi hiki, tunakutana na mzawa wa Ufaransa Eric Beloeuvre, aliyeacha raha za mjini na kwenda kufanya kazi katika misitu ya mkoa wa Gifu. (Kipindi hiki kilitangazwa Novemba 4, 2021.)
Eric Beloeuvre amekifanyia kazi chama cha ushirika cha misitu cha Nakatsugawa tangu mwaka 2019.
Eric anakata haraka miti ya urefu wa zaidi ya mita 20. Wakati mwingine anakata miti mingi hadi 40 kwa siku.