Upendo na Utamaduni Uliopikwa hadi kuwa Bora
Kazini nchini Japani ni kipindi kinachomulika maisha ya raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Japani. Katika kipindi hiki, tunakutana na Mkorea Kim Eun-young, ambaye masomo yake ya upishi yanavutia wanafunzi kutoka kote Japani. (Kipindi hiki kilitangazwa Januari 6, 2022.)
Kim Eun-young anaendesha shule ya lugha na upishi wa Kikorea mjini Kunitachi, Tokyo. Septemba 2020, alianza kutoa masomo mtandaoni kufuatia janga la korona.
Dhana ya shule ya Kim ni "Upishi wa mama nyumbani."
Oh Kyung-ah (kulia) anamsaidia Kim kuendesha shule hiyo. Wamekuwa marafiki kwa miaka 15.
Anayeichochea kazi ya Kim ni mama yake (kushoto).