Muuzaji Visu jijini Tokyo - Jeremy Escudero
Kazini nchini Japani inaangazia maisha ya raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini humo. Wakati huu, tunakutana na Jeremy Escudero, mzawa wa Ufaransa anayeuza visu vya jikoni katika duka lenye historia ya miaka zaidi ya 100 jijini Tokyo.
Jeremy Escudero (34) amekuwa akifanya kazi katika duka la visu vya jikoni tangu 2016.
Duka hilo lina visu karibu 1,000 vya maumbo, uzito na nyenzo mbalimbali. Jeremy anasikiliza hitaji la wateja kwa makini na kuchagua kisu bora.
Duka hilo lina toa huduma ya kunoa visu. Jeremy anafanyia mazoezi visu vya duka hilo ili kunoa ujuzi wake.