Mapenzi ya Mtunza Farasi kwa Familia Yake
Kipindi cha Kazini nchini Japani kinamulika maisha ya raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini humo. Wakati huu, tunakwenda uwanja wa mbio za farasi mkoani Kochi kukutana na Yerdy Bravo, mtunza farasi anayefanya bidii kuwafunza farasi ili kuisaidia familia yake katika nchi yake ya nyumani, Venezuela.
Yerdy Bravo mwenye umri wa miaka 32 amekuwa akiwatunza farasi kwenye uwanja wa mbio za farasi wa Kochi tangu mwaka 2019.
Akiyama Mami (kulia) kiongozi wa watunza farasi. Amejitolea kuhakikisha Bravo (kushoto) anapata usaidizi anaohitaji.