Mtengeneza Kahawa Asonga Mbele
Kutana na mwanamke Mkorea anayetayarisha espressos na aina mbalimbali za kahawa akiwa mhudumu mkuu katika mgahawa wa hoteli moja jijini Tokyo.  Kazini nchini Japani - ni kipindi kinachoangazia maisha ya watu kutoka kote duniani walioichagua Japani kama sehemu yao ya kazi.
Woo Youngju mwenye umri wa miaka 36 amekuwa mhudumu mkuu kwenye mgahawa wa hoteli eneo la Shibuya tangu mwaka 2017. Eneo la Shibuya ni kitovu cha tamaduni za vijana jijini tokyo.
Hatua muhimu kabisa ya kufanya kabla ya kuanza ni kujua ladha ya espresso. Hali ya buni hutofautiana kila siku kulingana na halijoto na unyevunyevu. Hivyo, ni muhimu kuondoa kwa uangalifu.
Kwa mijongeo mahiri ya mkono wake ulioshika jagi ya maziwa, maziwa yanatengeneza pambo maridadi la jani jeupe kwenye uso wa kahawia wa kahawa. Hii ni sanaa ya espressos.
Kominami Aya ni mkurugenzi wa upangaji wa huduma za chakula na vinywaji kwenye hoteli hiyo. Akitiwa hamasa na shauku ya Aya, Youngju aliamua kushiriki kazi ya kuandaa ufunguzi wa mgahawa huo.