Kuitambulisha Sake Duniani
Kipindi cha Kazini nchini Japani kinamulika maisha ya raia wa kigeni wanaofanya kazi Japani. Katika kipindi hiki cha leo, tunatembelea mji wa Tamba mkoani Hyogo magharibi mwa Japani ili kuangazia jitihada za kila siku za Kelley Kaminsky, mwanamke Mmarekani anayevutiwa na utengenezaji wa pombe ya sake. (Kipindi hiki kilitangazwa Julai 15, 2020.)
Kelley Kaminsky anafanya kazi katika kiwanda cha sake mjini Tamba, mkoani Hyogo.
Kelley (kushoto) anataka kuitambulisha sake kwa watu duniani kote; Mkuu wa kiwanda, Yashima Korei (kulia)anayesimamia utengenezaji wa sake.
Kelley anawathamini sana wafanyakazi wenziwe katika kiwanda hicho.