Kulenga kuwa Kundi Bora
Kipindi cha Kazini nchini Japani - ni dirisha la kutazama maisha ya watu kutoka kote duniani ambao wamechagua kufanya kazi nchini Japani. Wakati huu, tunakutana na Bijaya Acharya kutoka Nepal anayefanya kazi kama meneja wa baa ya mtindo wa Kijapani inayoitwa "Izakaya." (Kipindi hiki kilitangazwa Agosti 12, 2020.)
Bijaya Acharya ni meneja wa baa ya mtindo wa Kijapani katika eneo la Ginza, moja ya maeneo maarufu ya kibiashara lililopo katika eneo la mjini la Tokyo.
Bijaya anachoma yakitori, yaani mishikaki ya kuku, moja ya vyakula vya baa hiyo.
Kato Kota amekuwa akimsaidia Bijaya, mfanyakazi wa kwanza wa kudumu asiyekuwa Mjapani katika kampuni yake.
Bijaya na wafanyakazi wake walitunukiwa tuzo ya kundi bora la kazi na mwendeshaji wa baa hiyo.