Kwa Upendo wa Maisha na Vifaa vya Michezo ya Kunyanyua Vitu Vizito
Kutana na Mgiriki ambaye ni meneja wa kiwanda cha kutengeneza vifaa vya michezo ya kunyanyua vitu vizito. Kazini nchini Japani - kipindi kinachomulika maisha ya watu kutoka duniani kote walioichagua Japani kuwa sehemu yao ya kazi.
Mzawa wa Ugiriki, Anastasios Pappas mwenye umri wa miaka 37 amekuwa akifanya kazi katika kiwanda cha kutengeneza vifaa vya michezo ya kunyanyua vitu vizito katika kata ya Sumida mkoani Tokyo tangu mwaka 2010.
Anastasios ananyanyua vitu vizito vyenye jumla ya uzito wa kilo 60. Anastasios amewahi kunyanyua vifaa hivyo. Alishika nafasi ya pili katika mashindano ya kitaifa mwaka 2003 huko Ugiriki.
Uesaka Tadamasa, mmiliki na mkurugenzi mkuu mtendaji wa kampuni. Alizuru Ugiriki kikazi na kukutana na Anastasios aliyekuwa akifanya kazi ya kujitolea kwenye matukio ya mashindano ya kunyanyua vitu vizito. Wawili hao hatimaye wakawa marafiki.
Wanapokea oda za vifaa vyao kutoka duniani kote. Anastasios ana imani na anajivunia ubora wa bidhaa ambazo yeye na timu yake wanazitengeneza kwa ujuzi na uzoefu.